kabesejr blog
kabesejr
albino
Friday, April 27
DIAMOND NA JOKATE BILA KIFICHO NI LAIVUUUUUUUU
Kile kitendawili kwenye Wimbo wa Nimpende Nani wa mwanamuziki Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond Platinumz,’ kimeteguliwa na sasa siyo siri tena kuwa mkali huyo wa Bongo Fleva anatoka kimapenzi na Miss Tanzania namba 2, 2006/07, Jokate Mwegelo (pichani), Ijumaa limeshiba data.
Ama kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Habari inayotamba kwa sasa ni kuwa baada ya kujitahidi kuficha uhusiano wao kwa muda mrefu, mwanzoni mwa wiki hii uzalendo ulimshinda Diamond na kujikuta akiweka kweupe kuwa ni kweli Jokate ni wa kwake.
KWENYE MTANDAO WA BBM
Diamond alitumia mtandao wa BBM kuthibitisha kuwa anampenda Jokate kupita maelezo ambapo aliandika ‘No wan can take your place Kate..I love you so much my baby..’, jambo lililoibua mshtuko kwa waliyoona maneno ya Diamond ambaye bila shaka ndiye msanii namba moja kwa sasa Bongo.
HABARI ZASAMBAA
Baada ya Diamond kuweka maneno hayo, ghafla habari hiyo ilisambaa kama moto wa kifuu kwenye mitandao mingi ndani na nje ya Bongo huku ikipokelewa kwa hisia tofauti.
Kuna waliowapongeza na kuisifia ‘kapo’ yao lakini kuna walihoji kuwa mbona walikuwa wakibisha kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi huku Diamond akimuita Jokate dada.
“Watu tuliamini kuwa kitendo cha Jokate kushiriki kwenye video ya Wimbo wa Mawazo wa Diamond ndicho kilichomponza hadi kuhisiwa anatoka na staa huyo, tulidhani anaonewa kumbe ni kweli,” ilisomeka sehemu ya maoni ya mmoja wa watu waliobahatika kuisoma ‘status’ hiyo ya Diamond.
HUYU HAPA DIAMOND
Kutaka kuthibitisha kile alichoandika Diamond kwenye BBM na kusambaa mitandaoni, Ijumaa lilimvutia waya na kumuuliza ukweli wa habari hiyo ya kumwanika Jokate kuwa ni mpenzi wake ambapo kwa mara ya kwanza alikiri kutoka na mwanadada huyo akisema:
“Ni kweli niko in love (ndani ya penzi) na Kate (Jokate) ila bado sijapanga siku ya kumtambulisha rasmi kwa mashabiki wangu ili wamfahamu shemeji yao.”
MANENO MAZITO
Alipotakiwa kuthibitisha kile alichokisema kwa kutoa ufafanuzi wa ndani, Diamond alikatisha mazungumzo kwa kusisitiza: “Nampenda sana Jokate, hakuna wa kuchukua nafasi yake.”
JOKATE VIPI?
Kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa lilimtafuta Jokate ili kusikia neno lake juu ya kuwa ubavu wa Diamond lakini hakupatikana. Akipatikana naye atatoa neno lake.
TUMEFIKAJE HAPA?
Mwaka 2010 wakati Diamond alipozoa tuzo tatu za muziki za Kili, Ijumaa lilimnasa kwenye picha ya pozi na Jokate ambaye ni mwigizaji, modo na mtangazaji lakini alipoulizwa kama kuna kitu, alisema hakuna chochote kati yao (picha za tukio tunazo).
WEMA VS JOKATE
Mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa mchumba wa Diamond, Wema Isaac Sepetu alitangaza vita na Jokate akimtuhumu kumwingilia kwenye himaya yake ya kimapenzi.
KUTOKA IJUMAA
Timu ya Ijumaa inaamini kuwa ‘kapo’ ya Diamond na Jokate ni maua yanayopendezesha ulimwengu wa mastaa wa Kibongo hivyo tunawatakia kila la kheri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment