Elizabeth Gupta mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la BIG BROTHER AFRICA ambae kwa sasa anaishi Nigeria amethibitisha kwamba japo Marehemu Steven Kanumba ameshazikwa lakini mpaka jana bado taarifa za kifo chake zimeendelea kuzungumziwa nchini Nigeria.
Elizabeth amesema “mpaka sasa hivi ni kama ndoto, wengine wananitumia msg pia…….. kuna blogs nyingi wameandika habari zake na kuna watu wengi kutoka sehemu mbalimbali Africa wamekua wakitoa maoni yao kuhusu hicho kifo. blogs maarufu kama ya Ikeji, Radio na Magazeti ndio yameipa uzito sana habari ya kifo cha Kanumba”
hizo hapo chini ni Blogs mbalimbali kubwa za Afrika ambazo zimezungumzia sana taarifa za kifo cha Kanumba.
Source from Millard ayo official website
No comments:
Post a Comment