kabesejr blog

kabesejr

albino

Sunday, April 8

NINI KIMEMUUA KANUMBA?


Hadi sasa, Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inamshikilia msanii wa kike wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, kutokana na kifo cha Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia juzi.

Polisi katika Mkoa wa Kinondoni, wamesema wanaendelea na uchunguzi wa kifo cha nyota huyo kilichoitikisa Tanzania na kwa taarifa za awali, wanasema chumbani kwake ambako inaaminika ndiko umauti ulimkuta, walikuta panga, pombe ya Whisky ikiwa robo glasi pamoja na soda aina ya Sprite.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema vitu hivyo vilikutwa chumbani kwa Kanumba eneo la Vatican Sinza na kwamba wanaendelea kumhoji Lulu (18), mkazi wa Tabata Relini kuhusu tukio hilo, ambaye alikuwa chumbani pamoja na nyota huyo.

Kenyela alisema Kanumba alifariki juzi saa sita usiku nyumbani kwake ambapo kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Seth Bosco (24), ambaye ni msanii wa kikundi cha The Great Film Production, kaka yake alihitilafiana na Lulu, chanzo kikiwa ni simu.

Alisema Kanumba, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, aliingia chumbani kwake kujiandaa ili watoke, lakini baadaye kidogo aliambiwa na yeye aingie chumbani kwake kwani kuna mgeni anakuja na atakapokuwa tayari atamuita.

Alisema baadaye ndipo mdogo huyo wa marehemu alisikia kelele, kaka yake akimtuhumu Lulu kwa nini anawapigia simu mabwana zake wengine na ndipo ghafla aliitwa na msichana huyo na kuambiwa kwamba akamwangalie kaka yake amezidiwa.

Kenyela alimkariri mdogo huyo akieleza kwamba alipofika chumbani alimkuta Kanumba amelala sakafuni huku akitokwa na povu mdomoni na haongei, ambapo baada ya mawasiliano na daktari wake, alipofika aligundua kwamba alishafariki dunia.


                                                                      

2 comments:

master 1 said...

OOOOOOOOOOOOOOOOOH! POLENI SANA WASANII WA FILAMU TUKO PAMOJA KATIKA KILIO HIKI CHA MKALI WETU WA BONGO MOVE.
khamis said - ifakara - kilombero.

master 1 said...

kila msiba unaomuhusu mtanzania ni msiba wa watanzania wote, haijalishi hadhi yake nchini na ukiangalia watz wote ni ndugu. Mungu ailaze roro ya marehemu STEVE K, Big dady, Anko jj. mahali pema peponi.
Ameiin.
khamis k. said - ifakara.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...